Wednesday, December 2, 2015

 Pic 3
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga amesema kukutana na Akon nchini Marekani kumempa mwanga kimuziki.

Muimbaji huyo aliyerejea nchini kutoka Marekani, alikutana na Akon nyumbani kwake Los Angeles na kurekodi naye wimbo.


Akiwa huko, Mayunga amesema alipata mafunzo mengi ya muziki.

“Fursa hii imenipa mwanga zaidi  katika namna ya kufikiri na kujipanga ili kuzifikia ndoto zangu katika tasnia ya muziki,” amesema.

“Nimejifunza mambo mengi sana kupitia mafunzo niliyopata kutoka kwa Akon ikiwemo jinsi ya kukabili jukwaaa, namna ya kuchezea sauti yangu, mafunzo ya sauti,  namna ya kuandika na kutunga nyimbo na jinsi ya kuinua muziki wangu na kukuza kipaji changu kwa ujumla,” aliongeza.


0 comments:

Post a Comment