Wednesday, December 2, 2015

sloppy-handwriting-2
Haijalishi kama utaweza kuiongea kwa ufasaha au hukumbuki hata neno moja, lugha ya kwanza uliyojifunza ukiwa mtoto imeshaubadili ubongo wako kiasi ambacho hakuwezi kuwa na mabadiliko tena.

sloppy-handwriting-2

Watafiti wa nchini Canada wamebaini kuwa kusikia lugha ya kwanza enzi za utoto kunaathiri ubongo wa mtu na jinsi anavyokabiliana na lugha nyingine miaka mingi baadaye.

Hii hutokea hata kwa wale ambao hawajazungumza lugha yao ya kwanza katika maisha yao yote na hata kwa wale wanaomini kuwa wameisahau kabisa.

Watafiti wa McGill University and the Montreal Neurological Institute walifanya utafiti katika makundi matatu ya watoto wenye umri wa miaka 10 na 17 wenye historia mbalimbali za lugha.

Kundi moja liliundwa na watoto waliozaliwa na kukulia wakizungumza Kifaransa.

Watoto kwenye kundi la pili walikuwa wanazungumza Kifaransa na Kichina na la tatu liliundwa na watoto wa Kichina walioasiliwa kwenye familia za Kifaransa kabla hawajafikisha miaka mitatu na hawajawahi kuzungumza tena Kichina.

Watoto wote waliambiwa kutamka maneno sawa ya Kifaransa ambayo hayakuwa na maana yoyote kama ‘vapagne’ au ‘chansette.’

Wakati wa utafiti huo, watafiti walitumia kile kinachoitwa ‘functional magnetic resonance imaging’ (fMRI) kutazama maeneo yapi ya ungo yametumika.

Pamoja na makundi yote kufanya vizuri, fMRI ilibaini kuwa baadhi ya makundi yalikuwa tofauti kuhusiana na upande upi wa ubongo uliotumika.


0 comments:

Post a Comment