Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo,Anna Mgwira ambaye pia alikuwa mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ulioisha hivi karibuni,ameibuka tena na kumpa heko Dr Magufuli kwa kasi yake ya kukabiliana na maadui wakuu wa maendeleo.
Mgwira ambaye katika Uchaguzi wa mwaka huu ndiye aliyekuwa mgombea mwanamke pekee na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu nyuma ya Mgombea wa CHADEMA,Edward Lowassa,amesema kuwa amefurahishwa na kitendo cha Dr Magufuli kupambana hadharani na kwa dhati dhidi ya vitendo vya Rushwa na Ufisadi
NAPENDA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA NIA YAKE YA KUREJESHA MISINGI YA UTAIFA KWA KUKABILIANA NA MAADUI WAKUU WA MAENDELEO:RUSHWA NA UFISADI.
— annamghwiraofficial (@annamughwira) December 4, 2015

0 comments:
Post a Comment