WAZIRI
Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, ameingia matatani baada ya kudaiwa
kuvamia eneo la wazi na kuanza kuzungushia uzio, bila kufuata sheria na
utaratibu wa ujenzi.
Eneo
hilo la kiwanja namba 719/1/3 lililopo Mkiocheni, mtaa wa TPDC,
lilikuwa likitumika kwa ajili ya michezo, mikutano ya kisiasa, pamoja na
mikusanyiko mbalimbali ya kijamii.
Kufuatia
tuhuma hizo, timu ya maofi sa ardhi inachunguza uhalali wa umiliki
wake, hivyo wiki ijayo majengo yaliyojengwa kwenye eneo hilo yatavunjwa,
endapo ikithibitika kufanya uvamizi huo.
Mbali
na Sumaye, vigogo wengine wanaodaiwa wakuvamia kiwanja hicho ni
aliyekuwa Katibu Mkuu Mstaafu Ofi si ya Rais, Philemon Luhanjo pamoja na
Mbunge wa jimbo la Rungwe, Saul Amon, ambaye ni mfanyabiashara
anayemiliki maduka ya S.H. Amon.
Awali
kabla ya kuvamiwa kwa eneo hilo, ilielezwa kuwa iliyokuwa kampuni ya
High Precision Technology Centre (HPTCMatsutisha), kulilinda lisivamiwe
miaka ya 1970.
Hivyo
mikusanyiko mbalimbali za kimichezo, pamoja na shughuli za kisiasa
ilikuwa ikifanyika katika kiwanja hicho, ambako hata baada ya kampuni
hiyo kufa, ililiendelea kutumika kwa shughuli za kijamii.
MAZITO YAIBUKA
Uchunguzi
wa gazeti hili ulibaini kuwa, Sumaye anaendelea na ujenzi katika eneo
hilo bila kuweka kibao chenye kuonyesha wakandarasi wanaohusika na
ujenzi huo.
Lakini
pia, licha baadhi ya nyaraka kudai kuwa kiongozi huyo mstaafu
kulimiliki eneo hilo kuanzia mwaka 1998, hajawahi kulalamika kimaandishi
kwenye uongozi wa mtaa kuhusu shughuli zilizokuwa zikiendelea kwenye
eneo hilo.
Shughuli
hizo ni pamoja na uongozi wa serikali ya mtaa kuweka kifusi, ili
kusawazisha eneo hilo kuufanya uwanja utumike vizuri kwa ajili ya
michezo.
Aidha
wiki tatu zilizopita, Ofi sa Mtendaji wa Mtaa huo Mwanaidi Omary,
aliongozana na mmoja ya maofi sa wa ardhi wa Manispaa ya Kinondoni hadi
kwenye eneo hilo.
Ofi
sa huyo wa ardhi alitoa notisi ya mdomo na sio ya maandishi ya
kusitishwa ujenzi huo akidai mpaka mmiliki awasilishe nyaraka
serikalini.
Licha
ya ujenzi huo kufanyika bila kufuata taratibu za kisheria, ikiwemo
kutokuwepo kwa kibao kinachoonyesha mkandarasi anayehusika na ujenzi,
lakini ofi sa huyo hakuchukua hatua zozote za kisheria.
Katika
kutaka kujua ukweli wa mzozo huo, gazeti hili lilifanikiwa kupata barua
iliyoandikwa na serikali ya mtaa kwa Halamashauri hiyo kuhoji ujenzi
huo. Barua hiyo yenye kumbukumbunamba MKT/SER/MT/ TPDC/05/2015,
iliyoandikwa Desemba 11, mwaka huu na kupokelewa Desemba 14, bado
haijatolewa ufafanuzi na mkurugenzi kama ilivyokuwa ikielekeza.
LUKUVI KUTUMBUA JIPU
Kufuatia malalamiko hayo ya wananchi, Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema serikali itavunja uzio na shughuli za ujenzi zinazoendelea kwenye eneo hilo itakapobaini ukweli, ifi kapo Jumatatu.
Kufuatia malalamiko hayo ya wananchi, Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema serikali itavunja uzio na shughuli za ujenzi zinazoendelea kwenye eneo hilo itakapobaini ukweli, ifi kapo Jumatatu.
Katika kusisitiza hilo, Lukuvi alisema hatua hiyo itahusisha hadi vigogo wengine watakaobainika kuvamia eneo hilo.
Alisema baada ya serikali kupata taarifa, timu ya maofi sa ardhi itachunguza kwa kina eneo hilo ili kuthibitisha. Juzi gazeti hili lilishuhudia maofi sa hao wakiwa kwenye eneo hilo wakifanya uchunguzi.
CHANZO NA UHURU GAZETI
0 comments:
Post a Comment