Posted by Williammalecela.com on Thursday, December 24, 2015
Nchi tatu zenye maadili ya Kiislamu zimetangaza kuwekea wananchi wake marufuku ya sherehe za mwaka mpya.
Nchi hizo zilizochukuwa uamuzi huo wa
kuzuia sherehe za mwaka mpya ni Brunei na Tajakistan kutoka bara la
Asia, na Somalia kutoka bara la Afrika.
Sultan Hassanal Bolkiah wa Brunei, alitangaza marufuku
hiyo kutokana na kuwa kinyume na maadili ya Kiislamu, na kuweka adhabu
ya kifungo cha miaka 5 gerezani kwa raia watakaokiuka sheria.
Wizara ya elimu ya Tajakistan nayo ilitangaza kuweka marufuku ya miti ya mapambo ya Krismasi na sherehe za mwaka mpya ingawaje adhabu ya washerehekeaji haikubainishwa.
Kwingineko katika nchi ya Somalia, sherehe za Krismasi na mwaka mpya pia zilipigwa marufuku kwa madai ya kuwa ni misingi ya dini ya Kikristo.
Kiongozi mmoja wa wizara ya masuala ya
dini Mohammed Hayrow, alitoa maelezo na kusema kwamba watazuia sherehe
zozote zitakazofanyika kwa ajili ya Krismasi au mwaka mpya.
0 comments:
Post a Comment