Zanzibar tartiibu....
Disemba 20 mwaka huu 2015 Kamati ya Uongozi ya Chama cha ACT Wazalendo ilitoa tamko lake baada ya kufuatilia hali ya Zanzibar.
Moja ya mambo yaliyoelezwa katika tamko hilo ni uwepo wa askari wengi katika kisiwa hicho hali iliyokuwa inatishia amani kwa wananchi
Taarifa hiyo ya ACT mbali na masuala mengine, ikaeleza kuwa ni wakati muafaka kwa serikali kuhakikisha inawarudisha askari hao wa vikosi mbali mbali kuanzia jeshi la Polisi,JKU,KMKM JWTZ na Mafunzo katika makambi yao.
Lengo likiwa ni kuwaacha wananchi wakiwa katika uhuru wa kufanya shughuli zao wakati suala la mtanziko wa kisiasa kisiwani humo ukiwa unafanyiwa kazi
Kuanzia jana Disemba 22 na leo Disemba 23 majeshi hayo yameshaanza kuondoka katika maeneo mbali mbali ya mji wa Znz hali inayoashiria mwanzo wa mwisho mwema katika kadhia ya uchaguzi wa Zanzibar.
Ninaomba mamlaka husika ziendelee kufanyia kazi mapendekezo yetu mengine ili kulimaliza kabisa suala hili.

Zanzibar tartiibu.... Disemba 20 mwaka huu 2015 Kamati ya Uongozi ya Chama cha ACT Wazalendo ilitoa tamko lake baada...
Posted by Zitto Kabwe on 23 Disemba 2015

0 comments:
Post a Comment