Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy
Mwalimu ameagiza vituo vyote vya serikali vya kutolea huduma za afya
nchini, kwenye dirisha la mapokezi,vyumba vya madaktari na sehemu ya
dawa zinaandikwa "mpishe mzee kwanza apate huduma".
Agizo hili
linakwenda sambaba na uwepo wa madirisha ya wazee katika vituo vyote
vya serikali vya kutolea huduma za afya.
Mhe Ummy pia amehidi kupeleka Bungeni Mswada wa Sheria ya Taifa ya
Wazee ktk Bunge la mwezi Septemba ili kuhakikisha haki na stahili za
wazee nchini zinatekelezwa kikamilifu. Wazee walieleza kero zao kubwa ni
kupata matibabu, kutokuwa na kipato cha uhakika na vitendo vya
kudharauliwa na jamii.

0 comments:
Post a Comment