Posted by Williammalecela.com on Wednesday, December 30, 2015
Msanii nyota wa Bongo Fleva Nassib Abdul maarufu kama Diamond
Platnumz au SIMBA amefunguka juu ya ushiriki wa mama yake mzazi kwenye
video yake mpya ya Utaipenda.
Akizungumzia suala hilo Diamond Platnumz (SIMBA) amesema hakutegemea
kama mama yake mzazi angekubali kushiriki katika video hiyo maana
amekuwa akikataa hata kuhojiwa na vyombo vya habari kutokana na kutokuwa
huru akiwa mbele ya kamera.
Diamond ameeleza kufurahishwa kwake na mama yake kushiriki katika
video yake ya Utaipenda maana kusingekuwa na maana kama asingeshiriki
kwasababu amemtaja sana kwenye verse ya pili.
0 comments:
Post a Comment