Ndege iliyozinduliwa na Shirika la Ndege la Etihad
ilipowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam na kupokelewa na magari ya zimamoto kwa kumwaga maji kuashiria
uzinduzi rasmi wa Safari za ndege za shirika la ndege la Etihad lenye
makao makuu Abudhabi. Uzinduzi huo unatoa fursa sasa kwa watanzania
kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi kila siku.
Makamu wa Rais- Mauzo ya Kimataifa wa shirika la
ndege la Etihad Bw. Daniel Barranger akisalimiana na Balozi wa Umoja wa
falme za Kiarabu nchini Tanzania Mh. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi mara
baada ya uzinduzi rasmi wa shirika hilo uliofanyika katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijiji Dar es salaam. Uzinduzi huo
unatoa fursa sasa kwa watanzania kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es
salaam mpaka Abudhabi.
Makamu wa Rais- Mauzo Kimataifa wa shirika la ndege
la Etihad Bw. Daniel Barranger (kushoto) akijibu maswali ya waandishi
wa habari (hawapo pichani) mara baada ya uzinduzi wa shirika la ndege la
Etihad ambao ulifanyika siku ya jana jijini Dar es salaam.Pamoja nae ni
Mh. Balozi wa Umoja wa falme za Kiarabu nchini Tanzania Mhe. Abdullah
Ibrahim Al Suwaidi.
Mh. Balozi wa Umoja wa falme za Kiarabu nchini
Tanzania Mhe. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi akitoa hotuba yake kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya uzinduzi rasmi wa
shirika la ndege la Etihad uliofanyika katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijiji Dar es salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere mara baada ya uzinduzi rasmi wa shirika la ndege la
Etihad hapa nchini. Uzinduzi huo unatoa fursa sasa kwa watanzania
kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi kila siku.
Shirika la ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa za Falme za
Kiarabu, leo hii imeendelea kuimarisha uwepo wake Afrika Mashariki kwa
kuzindua huduma zake mpya za safari za ndege baina ya Dar es Salaam, mji
mkubwa zaidi nchini Tanzania na Abu Dhabi, mji mkuu wa Falme za kiarabu
(UAE).
Mara baada ya ndege inayozinduliwa kuwasili katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, ililakiwa na mizinga ya maji kama
ishara ya heshima kubwa na abiria walioshuka wakikaribishwa kwa burudani
ya ngoma za kitamaduni za Tanzania.
Shughuli ya kukata utepe ilifuatia ambayo katika kuweka kumbukumbu ya tukio hilo la kufana ambapo lilifanikishwa na
– Dr Shaaban Mwinjaka, Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi
– Dr Adelhelm James Meru, Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Maliasili
– H.E. Mbarouk Nassor Mbarouk, Balozi wa Tanzania Nchi za Falme za kiarabu
– H.E. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi, Balozi wa Nchi za Falme za kiarabu Tanzania
– Daniel Barranger, Makamu wa Rais wa Mauzo ya kimataifa wa shirika la ndege la Etihad
– Mhandisi:Thomas Haule Mkurugenzi Mamlaka ya Ndege
Dar es Salaam imekuwa ni kituo cha tatu kwa shirika la ndege la
Etihad Afrika Mashariki, baada ya Nairobi na Entebbe,na ya tisa barani
Afrika.
Huduma hii mpya ikiwa inaendeshwa na ndege aina ya Airbus A320
yenye madaraja mawili, siti 16 daraja la “Business” na siti 120 daraja
la “Economy” ikiwa imelenga wafanya biashara na wanaosafiri kwa starehe
moja kwa moja kila siku baina ya Dar es salaam na Abu Dhabi, pamoja na
uunganishaji mrahisi kwenda nchi nyingine ukanda wa GCC, Ulaya, India,
Asia kaskazini, Asia ya Kusini na Australia.
Bw. Barranger, alisema “uzinduzi huu wa safari za shirika la
ndege la Etihad kuja Dar es Salaam zimewiana na mkakati wetu wa kulenga
masoko yanayo endelea kukua kwa kasi”.
“Dar es Salaam ni mji ambao umekuwa kivutio sana kwa watalii
wanaotaka kufahamu tamaduni na historia ya Tanzania, pia ni mlango wa
vivutio vya kitalii vingi vya kitaifa na kimataifa ikiwemo mlima
Kilimanjaro, mbuga za wanyama kama Serengeti na kisiwa cha Zanzibar.
“Nchi Falme za kiarabu ni mdau mkubwa wa kibiashara na
Tanzania, huduma hii mpya itaongeza nguvu ushirikiano wa kibiashara
baina ya nchi hizi mbili. Ratiba za safari za ndege zitawapa wageni
urahisi wa kupata ndege za kuunganisha safari kwenda nchi nyingine,
ikiwa inahudumia safari nyingi sana baina ya Tanzania na nchi nyingi
katika mtandao wetu wa kimataifa kama Ahmedabad na Mumbai nchini India
au Beijing na Shanghai nchini China.”
“Pamoja na kutoa huduma ya moja kwa moja kwa watalii na wafanya
biashara baina ya nchi hizi mbili, safari hizi pia zimeendelea
kuimarisha uwepo wetu Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla” aliongezea.
Shirika la ndege la Etihad limekuwa likiongeza uwepo wake
barani Afrika tokea walipozindua safari zake za kwanza barani Afrika,
huko Cairo November 2004. Baada ya hapo zikafuatia Casablanca, Entebbe,
Johannesburg, Khartoum, Lagos, Nairobi, (15 January 2015) na Mahe huko
visiwa vya shelisheli na mipango ya uzinduzi katika mji wa Rabat,
Morocco katikati ya mwezi Januari 2016.
Ratiba za shirika la ndege la Etihad, Dar es Salaam kuanzia tarehe 1 December 2015:
Flight No.
Kutoka
Kuondoka
Kwenda
Kufika
Idadi
Ndege
EY681
Abu Dhabi (AUH)
8:20
Dar es Salaam (DAR)
13:00
Kila Siku
A320
EY682
Dar es Salaam (DAR)
13:50
Abu Dhabi (AUH)
20:15
Kila Siku
A320
Zingatia: Muda wa kuondoka ni majira ya Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment