Kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Jeshi la Polisi kupambana na
ujangili, kimemtia mbaroni mlinzi wa mfalme wa Qatar, kwa tuhuma za
kusafirisha fuvu la twiga kwenda Uarabuni.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani jana
alithibitisha kukamatwa kwa mlinzi huyo wa mfalme na kwamba utaratibu wa
kumfikisha mahakamani ulikuwa ukifanyika.
“Ni kweli tuna mtu kama huyo tulimkamata pale (Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro) Kia, akapelekwa Arusha lakini amerudishwa
Moshi na mchakato wa kumfikisha mahakamani hapa Moshi unaendelea,”
alisema Ngonyani.
Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji na Idara ya
Wanyamapori zimemtaja mlinzi huyo kuwa ni Jasim Mbarakke Alhkubaisi
(43).
Mlinzi huyo alikamatwa wakati mtuhumiwa muhimu aliyepatikana na hatia
ya kusafirisha wanyama hao wakiwamo twiga wane kwenda jijini Doha,
Qatar, Kamren Ahmed akiwa hajapatikana licha ya kushtakiwa na kuhukumiwa
kifungo baada ya kupatikana na hatia

Hakuna kucheza na mali ya taifa....we don't give a damn kuwa ni mlinzi wa mfalme eti kisa ni mwarab, hizo zama za Kikwete ya wewe mwarab jichukulie tu zimekwisha. Kamata jambazi, choma maji ya moto na tupilia kule. Mbongo anakamatwa uarabuni anakatwa mkono, kwanini na huyu mwizi asiuliwe kwa style ya mob justice ya huku uswazi? Tuleteeni jamani, mwizi ni mwizi tu hana haki.
ReplyDelete