Picha ya kipimo cha X-ray ikionesha simu na chaja zikiwa
zimesagwasagwa ndani ya tumbo la mfungwa huyo.
MFUNGWA mmoja (hakufahamika jina lake) nchini Brazil amemeza simu ya mkononi na chaja zake
mbili wakati akijihami na kukataa kuingizwa gereza la Papunda liliyopo mji mkuu
wa nchi hiyo, Brasilia.
Tukio hilo lilitokea juzi
wakati mfungwa huyo na wengine waliporuhusiwa kwenda kutembelea ndugu na jamaa
zao wakati wa Siku ya Watoto nchini Brazil ambayo inasherehekewa na
familia nyingi zaidi nchini humo kuliko sikukuu yeyote kiutamaduni na kiuchumi.
Siku hiyo watoto hupewa zawadi mbalimbali na wanafamilia wao.
Vipimo vya mionzi kwa njia ya X-rays vimeonesha kuwa simu na
chaja hizo tayari vimeharibu vibaya sehemu ya utumbo wake, juhudi mbadala za kuweza kunusuru maisha yake
zimeendelea kufanywa na madaktari. Taarifa zaidi zinasema kuwa mbali na
mtuhumiwa kutenda tukio hilo,
amerudishwa rumande japo haijafahamika hapo mwanzo alikuwa amefungwa kwa kosa
gani.
Gavana wa gereza hilo
amesema kuwa mfungwa huyo atapoteza haki za msingi alizokuwa nazo hapo mwanzoni
na sasa atapewa adhabu kwa kosa jipya alilofanya la kumeza simu ya mkononi na
chaja. Mnamo Agosti 11, 2000 wafungwa watano walifariki dunia na wengine tisa
kujeruhiwa wakati askari wakituliza
ghasia kwenye gereza hilo la Papuda ambapo Oktoba 2001 watu wawili walikufa na
wengine 11 kujeruhiwa kwenye tukio kama hilo.

0 comments:
Post a Comment