STAA wa Hip Hop, Kanye West amefanya kufuru baada ya kutoa kiasi cha
dola milioni 1 (zaidi ya bilioni 2 za Kitanzania) ikiwa ni shukrani kwa
mke wake kumpatia mtoto wa pili.
Kanye alifanya hivyo hivi karibuni ikiwa ni siku chache tangu Kim ajifungue mtoto wa kiume aliyemuita jina la Saint West.
Kwa mujibu wa Jarida la People la Marekani, Kanye humwambii chochote
juu ya ujio wa mtoto wake huyo na kwamba amekuwa akimhudumia Kim kama
vile malkia.
“Tangu Kim amejifungua amekuwa ni mchovu sana kwani bado anamaumivu
makali ambayo hayaelezeki na ndiyo maana Kanye anafanya kila liwezalo
awe karibu na Kim na kumsaidia kila kitu kama malkia anavyofanyiwa,”
iliandika sehemu ya jarida hilo.
Kim na Kanye walifunga ndoa Mei mwaka huu pande za Paris, Ufaransa na
kisha kuhamishia sherehe pande za Italia. Wawili hao wamebahatika
kupata watoto wawili ambapo wa kwanza ni wa kike anaitwa North West na
wa pili wakiume, Saint West.

0 comments:
Post a Comment