Mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Alhaji Abubakari Zuberi ameivunja mamlaka ya uendeshaji na usimamizi wa msikiti mkuu wa mkoa wa Arusha na kuweka mamlaka mpya ili kuimarisha utendaji.
Akitangaza maamuzi hayo kwa niaba ya mufti Sheikh mkuu wa mkoa wa
Arusha Shabani Juma amesema anaamini kuwa mamlaka mpya iliyowekwa
itafanya kazi kwa ufanisi na kwa kasi ya hali ya juu pamoja na kujipanua
ili kwafikia waumini wengi kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya
kuwahudumia kwa ukaribu.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa mamlaka
iliyovunjwa wamesema kuwa hawajaridhishwa na uamuzi huo kwani
hawakushirikishwa wakati wa vikao vya maamuzi vya mkoa vilivyojadili
majina kumi na tano ya wajumbe yaliyotumwa kwa mufti kwa ajili ya uteuzi
huo wa mamlaka mpya.
Kwa upande wao wajumbe wapya waliochaguliwa kuingia katika mamlaka
hiyo mpya wamesema kuwa wanachangamoto kubwa ya kuwaunganisha waumini
pamoja na viongozi wao ili kuleta maendeleo na kudumisha mshikamano.

0 comments:
Post a Comment