Wakati huo huo Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ametua nchini
Pakistan kwenye ziara ya kushtukiza ambapo amekutana na mwenzake Nawaz
Sharif.
Bw Modi alikuwa safarini kurejea India kutoka Afghanistan alipoamua
kutua katika mji wa mashariki wa Lahore. Ziara yake imelingana na siku
ya kuzaliwa ya Bw Sharif.
Bw Modi ndiye waziri mkuu wa kwanza wa India kuzuru Pakistan tangu 2004.
Bw Modi ndiye waziri mkuu wa kwanza wa India kuzuru Pakistan tangu 2004.
Mataifa hayo yamepigana vita mara tatu tangu kujipatia uhuru kutoka
kwa Uingereza, vita vivili kuhusu jimbo la Kashmir, kila moja likidai
umiliki wa eneo lote la Kashmir, mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 60
sasa.
0 comments:
Post a Comment