Mgombea mtarajiwa wa uraisi kupitia
chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump ametaka Waislamu
kuzuiwa kuingia nchini Marekani kwa muda.
Trump anasema utafiti
uliofanywa hivi karibuni unaonesha kuwa waislamu wengi wamepandikiza
chuki juu ya Marekani na sasa mpaka uongozi ubaini sababu za kuwepo kwa
chuki hiyo, watu wanahitaji kujilindwa.
Ikulu ya Marekeni imesema tamko la Trump linaenda kinyume na maadili ya taifa la Marekani na maslahi ya usalama wa taifa.
Tamko
hilo la Donald Trump limekuja siku chache baada ya watu kumi na nne
kuuwawa katika shambulio la risasi zilizopigwa katika mkusanyiko wa watu
na wanandoa ambao ni Waislamu.
Shirika la kijasusi la Marekani
FBI limesemaSyed Farook na Tashfeen Malik walipandikizwa itikadi kali
lakini hawajui na nani na ni kwa namna gani.
FBI
walioko California,wameivamia nyumba inayoshukiwa kuhusika katika
shambulio hilo na kusema imepata mabomba kumi na tisa ambayo yangeweza
kutumika kutengenezea mabomu katika nyumba yao iliyoko Redlands huko
California.
Vyombo vya habari vya Marekani vinasema nyumba hiyo ni
ya rafiki ambaye anaaminika kuwa alifanya manunuzi ya bunduki
zilizotumika katika shambulio
STORY NA BBC

0 comments:
Post a Comment