Sunday, December 13, 2015


 
 
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi  William Ole Nasha amesema kuwa hatamwangusha Raisi John Pombe Magufuli na Watanzania kwa kuhakikisha kuwa anawajibika na kufanya kazi kwa bidii na kuleta mabadiliko katika sekta hizo .
 
Nasha ambaye uteuzi  huo ulivyotangazwa rasmi kwenye vyombo vya habari ulimkuta katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro hali iliyowashangaza wengi kwani hawakuwa wametarajia kuwa uteuzi huo ungetokea.
 
Akizungumza katika baraza la Madiwani Nasha alishukuru kwa uteuzi huo na kuahidi kuwa hatawaangusha Watanzania  kuwa hana rekodi ya kukosa maadili.
 
“Umakini mkubwa umetumika kuteua baraza la Mawaziri mpaka leo hii Mheshimiwa Raisi hajamaliza kuteua baraza , ni heshima kubwa sana kwangu namshukuru Magufuli kwa dhamana hii kubwa “ Alisema Nasha
 

0 comments:

Post a Comment