Sunday, December 27, 2015

 

Waziri wa  nchi sera uratibu na bunge, ajira na walemavu  Mheshimiwa  Jenista Mhagama amewatembela na kuwafariji waathirika wa majanga  ya mvua zinazoendelea kunyesha ambazo zimeharibu nyumba za wananchi, kuwajeruhi na kuwaacha hawana mahali pakuishi mkoani Ruvuma

 maeneo yaliyotembelewa na waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma Mheshimiwa Jenista Mhagama  ni pamoja na kata ya magagura ambapo ametoa msaada wa shilingi laki tisa kwa kata hiyo na kata ya Mbinga Mharule zilizokumbwa na maafa huku Bi. Bertha Komba na mwanae mdogo wakinusurika kufa baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao ambapo kufuatia maafa hayo ameagiza kupandwa kwa miti ili mkujikinga na upepo.
 
Waathirika wa maafa hayo akiwemo mlemavu mmoja wa miguu anayetambaa aliyeangukiwa na ukuta wanaeleza hali ilivyokuwa na namna walivyoweza kujinasua

0 comments:

Post a Comment