Posted by Williammalecela.com on Monday, December 21, 2015
Staa maarufu wa filamu Bongo, Aunty
Ezekiel amefungua kinywa chake na kusema kuwa kwa sasa yuko kwenye
mchakato wa kumtafuta mdogo wake na Cookie kwa kuwa hataki kukaa muda
mrefu ili kupata mtoto mwingine.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii
hivi karibuni Aunty,alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa kuwa anaona
kuzaa mapema na kumaliza ndiyo poa ili aweze kuendelea na kazi zake
vizuri kuliko kukaa muda mrefu halafu ndiyo ubebe ujauzito tena.
“Sasa
hivi mimi na baba Cookie tumeshaamua kufanya maamuzi mazuri kabisa ya
kuongeza mtoto mwingine maana tumeona kwanza ndiyo furaha yetu kubwa na
kitu kingine tukizaa haraka ni vizuri zaidi tunaweza kufanya kazi zetu
kwa ajili ya kusomesha na si kufikiria kuzaa tena,” alisema Aunty.
0 comments:
Post a Comment