MOYONI
nina majonzi, sina tofauti na mpofu! Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ au
‘Lady Jaydee’ kwa sasa hana makazi maalum Bongo, amehamishia makazi na
shughuli zake katika ardhi ya ‘Kansela’ wa Ujerumani, Angelina Merkel
kwenye Jiji la Born.
Katika mazungumzo yake na
mwandishi wetu kwa njia ya simu, Jumatatu ya wiki hii, Jide ambaye
alidai kwa sasa yupo nchini kwa Sikukuu ya Krismasi (kesho), alisema
sababu zilizomfanya akapige kambi nchini humo ni kuchoshwa na maneno ya
watu ambao kazi zao ni kutazama nani kafikwa na baya ili waeneze sumu ya
maneno.
Kwa sauti ya ‘kibabe’ na yenye mamlaka, Jide
alisema: “Lakini ukiachana na Ujerumani, wakati mwingine natumia muda
mwingi kuwa nchini Afrika Kusini (Sauzi) kwa mizunguko ya kimaisha na
kupumzisha akili yangu.”
UJERUMANI ANA NYUMBA?
Jide:
“Kwa sasa naishi hotelini, lakini kuna marafiki na jamaa zangu ambao
wako kule. Kwa hiyo sina shida. Muhimu ni kukaa mbali na maneno ya watu
wafurahiao matatizo ya wengine.
Kila mtu anageuka adui,
ukiwa na mafanikio makubwa, watu wanajisogeza karibu, ukipungukiwa na
jambo, haohao wanaanza maneno na kukusema vibaya, maisha hayatabiriki.”
HATAKI KUSIKIA MAPENZI!
Amani: “Vipi kuhusu mumeo, Gardner Habash, una mpango wa kurejeana naye?”
Jide:
“Sitaki kusikia kabisa mambo ya mapenzi. Sitaki na usiendelee kuuliza
upuuzi kama huo tafadhali. Si tu kwa huyo mtu (Gardner), hata kwa awaye
yeyote, sitaki kusikia.”
ASIULIZWE KUHUSU MALI ZAKE!
Amani
lilimuuliza Jide kuhusu ukweli juu ya madai kwamba amefilisika na
kufikia hatua ya baadhi ya nyumba zake kuwa katika hatihati ya kupigwa
mnada.
Jide: “Sitaki kugusia mambo hayo. Hata hivyo,
umebahatika sana kupokelewa simu na kuzungumza na mimi, licha ya kuwa
umejitambulisha unatoka Global. Sipendi mazungumzo na waandishi, hususan
nyie wadaku.”
KUHUSU MUZIKI?
Jide: “Siwezi kusema nimeacha muziki, nipo maana ndiyo kazi pekee iliyonitambulisha.
Nawaasa
mashabiki wangu waendelee kiniunga mkono, nawapenda sana na bila wao
hakuna Jide. Lakini kwa sasa kuna mambo nayaweka sawa nje ya muziki.”
YUPO DAR AU KWINGINEKO?
Jide: “Kwa sasa niko Dar (Jumatatu), lakini keshokutwa (jana
Jumatano)
nitakuwa nyumbani Musoma kwa ajili ya Krismasi. Niko kwenye mapumziko
maalum ya sikukuu hiyo, lakini baada ya hapo, nitaendelea na mambo yangu
mengine, ikiwemo kurejea Ujerumani.”
Chanzo: Global Publishers

0 comments:
Post a Comment