MAHAKAMA Kuu ya nchini Panama, imeamuru kukamatwa kwa Rais wa zamani
wa nchi hiyo, Ricardo Martinelli (pichani), aliyeongoza nchi hiyo kwa
kipindi cha miaka sita kuanzia 2009.
Sababu ya amri hiyo ni kutokana na mashtaka yaliyokuwa yakimkabili ya
kutumia fedha za umma kinyume na utaratibu akiwa madarakani ili kufanya
upelelezi kwa takriban watu 150 maarufu nchini mwake.
Miongoni mwa waliodaiwa kudhurika na upelelezi huo uliofanyika
kinyume cha sheria ni pamoja na wafanyabiashara, wanasiasa, wanasheria,
madaktari pamoja na wanachama wa umoja wanaharakati wafanyabiashara.
Hata hivyo, Rais mstaafu Martinelli alikana mashitaka hayo kwa kusema
kuwa ni moja ya njama za kumchafua zinazofanywa na Rais wa nchi hiyo
aliyeko madarakani, Juan Carlos Varela.
Taarifa zinasema Mahakama imefi kia uamuzi wa kumkamata Martinelli
baada ya kushindwa kutokea mahakamani mwanzoni mwa mwezi huu, kwa ajili
ya shauri la kwanza.
Kutokujitokeza kwake mahakamani kunasemekana ni kwa makusudi kwa kuwa anaishi mji wa karibu na mahakama hiyo jimbo la Miami.

0 comments:
Post a Comment