Wednesday, December 23, 2015


 MANDERA, Kenya

SIKU moja baada ya tukio la watu wenye silaha waliosemekana kuwa wa kundi la Al-Shabaab kuvamia na kulishambulia kwa risasi basi la abiria la kampuni ya Makkah, kwa lengo la kuwauwa abiria wa dini ya kikristo, imebainika kuwa wanawake wa kiislamu waliwaokoa wakristo kwa kuwafunika na Hijab.


Mmoja wa abiria aliyenusurika kifo katika shambulio hilo la basi lililofanyika juzi eneo la Mandera, aliviambia vyombo vya habari vya kimataifa kuwa wanawake wa Kiislamu walivua hijab na kuwastiri wanawake wakikristo ili kuwaokoa wasiuawe.

Abiria huyo ambaye ni Mwalimu kitaaluma, alijeruhiwa wakati wa shambulizi hilo la alfajiri na kusema kuwa mara baada ya basi hilo kutekwa, Magaidi hao waliwaeleza kuwa waislamu wote wako salama.


“Walituambia kuwa sisi waislamu tulikuwa salama na hivyo tukagundua kuwa wanawalenga wakristo, hapo ndipo wanawake tukavua hijab zetu na kuwavalisha wanawake wakikristo ili kuwaepusha na kifo,” alisema.

Aidha alisema kwa kuwa wapiganaji hao walikuwa wanaume, wanawake walijitenga na kuwafi cha wanawake wakristo na hivyo kuwaokoa wasiuawe kwa kuwa hakukuwa na ukaguzi wa kuwavua hijab.

Kutokana na hatua hiyo, idadi ya waathirika ilikuwa ndogo kufuatia jitihada za abiria waislamu kuwafi cha na kuwaokoa wenzao wakristo waliokuwa wakisafi ri pamoja.

Tukio hilo limevutia hisia za wengi kote duniani ambapo watu wa kada mbalimbali waliusifu umoja huo ulioweka pembeni imani za kidini ambazo kwenye baadhi ya maeneo zinaleta mtafaruku mkubwa.

0 comments:

Post a Comment