RAIS John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Seneti
na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Burundi, Reverien Ndikuriyo Ikulu jijini
Dar es Salaam kuhusu hali ya kisiasa na usalama nchini Burundi na
jitihada zinazochukuliwa na Tanzania, ikiwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC).
Akiwasilisha ujumbe wa Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi kuhusu hali
ya Burundi, Spika Ndikuriyo alisema Serikali ya Burundi ipo tayari
kufanya mazungumzo na wadau wote wa siasa kuhusu hali ya nchi hiyo na
jitihada za kuumaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.
Akitoa maelezo ya kikao hicho kwa niaba ya Dk Magufuli, Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa,
Balozi Dk Augustine Mahiga alisema Serikali ya Burundi imekubali
usuluhishi, unaofanywa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa niaba ya
Marais wa EAC kutokana na kikao kilichofanyika Dar es Salaam Julai mwaka
huu na kwamba Serikali ya Burundi iko tayari kushiriki mazungumzo hayo
ya amani.
“Nimeagizwa nipeleke taarifa kwa mawaziri wa nchi za nje wa nchi
jirani juu ya maandalizi ya mazungumzo hayo ambayo yataanza kule Uganda
tarehe 28 mwezi Desemba”, alisema

0 comments:
Post a Comment