Thursday, December 10, 2015

Zitto Kabwe afunguka,
 
Baadhi ya Watanzania wenzangu wamehoji kuhusu kwamba nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, kwanini sikuona 'majipu'
ya Mamlaka ya Bandari, Mamlaka ya Mapato nk. 1) nawashukuru kwamba wanatambua kazi kubwa tuliyofanya tukiwa PAC. Ile kuhoji tu ni ishara kubwa sana kwamba watathamini mchango wetu 2) PAC ni kamati inayofanyia kazi Taarifa ya CAG. PAC haiibui mambo yake na ikitaka kufanya hivyo lazima iitishe ukaguzi maalumu.

 PAC sio 'executive', sio 'internal auditor' na sio 'external auditor'. PAC ni Kamati ya Usimamizi ( oversight) . 3) PAC katika ripoti zake mbalimbali iliibua suala la ukwepaji kodi na kuonyesha kuwa Idara ya Forodha hupoteza mapato ya tshs 900 bilioni kwa mwaka kwa kutumia takwimu za 2013/14. Ripoti hii ilijadiliwa Bungeni. Ni wajibu wa Serikali kutekeleza mapendekezo ya Kamati na sio wajibu wa kamati ya Bunge kushtaki, kuendesha mashtaka na kuhukumu 4) PAC iliibua masuala ya TPA na kuwasilisha ripoti Bungeni na kujadiliwa.

Watanzania waelewe majukumu ya Kamati za Bunge na mipaka yao. Tunaunga mkono hatua za kupambana na ufisadi. Tunaomba Haki itendeke.

0 comments:

Post a Comment