MKUU wa Polisi nchini Inspekta Jenerali (IGP) Ernest Mangu amekanusha
kufutwa kazi kwa askari kadhaa wanaodaiwa kuwa na vyeti feki kama
iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii juzi na akasema Jeshi lake
linamtafuta mtu ambaye amesambaza taarifa hizo alizoita za uzushi.
IGP
Mangu alisema jana kuwa taarifa hizo sio za kweli na jeshi lake
halikusambaza taarifa hizo hivyo wanamtafuta kwa udi na uvumba mtu
aliyesambaza taarifa hizo za uwongo na akajifanya ni Jeshi la Polisi.
“Taarifa hizo sio za kweli na tayari msemaji wa Polisi jana (juzi)
alishazikanusha kupitia hiyo mitandao ya kijamii.Nasisitiza kuwa
tunamsaka aliyesambaza taarifa hizo za uwongo,” alisema IGP Mangu wakati
anajibu maswali ya waandishi wa habari jana.
Juzi kwenye
mitandao ya kijamii kulipositiwa majina ya askari Polisi wengi wenye
vyeo vya chini na vya kati wakidaiwa kuwa wamefukuzwa kazi baada ya
kubainika kuwa walijipatia ajira hiyo kwa kutumia vyeti bandia.

0 comments:
Post a Comment