Na Modewjiblog team, Singida
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone ofisini kwake kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mkoani humo.
Mratibu huyo yupo Mkoani hapa kwa siku mbili kukagua miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Katika siku yake ya kwanza atatembelea mradi wa afya ambao unashughulikia watu wanaoishi na VVU katika kijiji cha Puma wilaya ya Ikungi. Pia atatembelea kikundi cha ufugaji nyuki kinachojihusisha na uzalishaji wa asali na utengenezaji wa mishumaa.
Aidha akiwa kijiji cha Puma atatembelea kambi waliokolazwa watu wenye ugonjwa wa Kipindupindu.
Katika ukaguzi wa miradi hiyo Mratibu huyo atapata nafasi ya kuzungumza na walengwa wa miradi hiyo ili kupata mafanikio na changamoto zilizojitokeza.
Katika siku yake ya pili na ya mwisho mkoani Singida Bw. Alvaro Rodriguez atatembelea mradi mkubwa wa ufugaji nyuki kisasa unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP).
Baada ya hapo atatembelea ujenzi wa hospitali ya rufaa inayoendelea kujengwa kijiji cha Mandewa nje kidogo ya mji wa Singida.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone alitoa Shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa misaada yake ya kuisaidia serikali katika kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Hata hivyo ameomba Mashirika hayo yaendelea kusaidia katika Nyanja za upatikanaji wa ajira kwa vijana na masoko kwa wakulima.
Mratibu huyo baada ya kumaliza ziara yake mkoani Singida ataelekea mkoa wa Tabora ambapo ataanza ziara yake tarehe 3 mwezi Desemba na baada ya kumaliza mkoa wa Tabora atelekea mkoani Kigoma tarehe 4 hadi 6 nwezi Desemba.
Singida ni kati ya mikoa itakayounufaika na mpango mpya wa malengo ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals-SDGs) unaotarajiwa kuanza kutekelezwa 2016-2030.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone akisalimiana na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kulia) aliyeambatana na Bw. Rodriguez. Aliyeketi ni Katibu Tawala wa mkoa wa Singida,
0 comments:
Post a Comment