Rais John Magufuli
Mwanza. Chama cha Albino Tanzania (Tas) Mkoa wa Mwanza, kimemuomba Rais John Magufuli atumie nafasi zake kumi za uteuzi kuchagua wabunge wenye ulemavu ili Bunge liwe na sauti ya kuwatetea.
Mwenyekiti wa Tas mkoani hapa, Alfred Kapole alisema juzi kuwa ili
sauti za watu wenye ulemavu zisikike kwa nguvu ni vyema Bunge likawa na
wabunge wengi wenye ulemavu.
“Tunamwomba Rais Magufuli kupitia nafasi zake 10 za uteuzi wa
wabunge, ateue wabunge wenye ulemavu ili na sisi matatizo yetu
yawakilishe na kusikika kwa nguvu kubwa tofauti na ilivyo sasa,” alisema
Kapole na kuongeza:
“Tunapata tabu kwenye miuondombinu iliyopo, tunaomba hili nalo
aliangalie kwani walemavu tumekuwa tukipata shida hasa tunapohitaji
huduma kwenye baadhi ya ofisi.”
Vilevile, Kapole alisema wanafahamu kuna hukumu zilizotolewa kwa watu
waliohusika na mauaji ya albino, lakini hazijatekelezwa, hivyo
wanamwomba Rais kushughulikia kwa kina.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania
(Shivyawata), Felician Mkude alisema albino wanahitaji uangalizi kwani
wamekuwa wakiuawa kwa imani za kishirikina na kwamba vitendo hivyo
vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku.
“Vitendo hivyo kwenye makaratasi vinaonekana vinapungua, lakini
vinaongezeka kila siku, tunavyoviona haviripotiwi kwa wingi,” alisema
katibu huyo.
Source;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment