Makaburi matatu yanayotembelewa sana na watu jijini Moscow yatawekewa huduma ya mtandao ya wi-fi.
Wanaotembelea
makaburi hayo wataweza kutumia mtandao wa intaneti bila malipo katika
makaburi ya Novodevichy, Troyekurovskoye na Vagankovo kuanzia mapema
2016 kwa mujibu wa tovuti ya Moscow City.
Mkuu wa huduma za
makaburi mjini Moscow Artem Yekimov anasema lengo ni kusaidia wageni
kwenye makaburi hayo kutafuta habari zaidi kuhusu watu mashuhuri
waliozikwa humo.
Aidha, kuwafanya wafurahie matembezi yao makaburini.
Kampuni
ya mawasiliano ya YS System inasema ilijitolea kuweka huduma ya wi-fi
humo baada ya kusikia mipango ya kutenga maeneo ya watu “kutulia
kisaikolojia” katika makaburi hayo.
Makaburi ya Novodevichy ni moja ya maeneo yanayotembelewa sana na watalii Moscow.
Miongoni
mwa watu waliozikwa humo ni mwandishi Anton Chekhov, kiongozi wa zamani
wa muungano wa Usovieti Nikita Khrushchev na rais wa zamani wa Urusi
Boris Yeltsin.

0 comments:
Post a Comment