MAHAKAMA
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imetoa wiki moja kwa upande wa
Jamhuri katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na
aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM),
kuwasilisha majibu yao.
Jaji Ama –Isario Munisi, alisema
hayo jana mahakamani hapo, wakati shauri hilo lililofunguliwa na Mtemvu
dhidi ya wadaiwa watatu akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),
lilipokuja kwa kutajwa.
Wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke na Mbunge wa Jimbo hilo, Abdallah Mtolea (CUF).
Jaji alisema upande wa Jamhuri
unatakiwa kuwasilisha majibu yao Desemba 21, mwaka huu na upande wa
wadai uwasilishe majibu yake Desemba 24, mwaka huu.
Alisema shauri hilo litatajwa
Desemba 29, mwaka huu, kuangalia iwapo pande zote husika zimewasilisha
majibu yake ili kupanga tarehe ya usikilizwaji.
Awali, Wakili wa Mtemvu, Egidi
Mkoba, alidai Mtolea hayupo lakini mara ya mwisho alikuwepo na alikuwa
anajua kama kesi inakuja jana.
Jaji alisema shauri lilikuja kwa
kutwaja, ambapo alihoji utaratibu unaotumiwa na upande wa Jamhuri kwa
sababu bado haujawasilisha majibu yake.
Wakili wa Serikali Mkuu, Ponsiano
Lukosi kwa niaba ya wadaiwa, alidai anaendelea kujibu na pia wanaendelea
kupata maelekezo kutoka kwa mdaiwa wa kwanza na wa pili kwa kuwa
wanavielelezo vingi ambavyo lazima avisome na kujibu.
Jaji aliutaka upande wa wadaiwa kufuatilia kwa kuwa hawezi kwenda likizo kabla ya usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo.
Lukosi alidai atalifanyia kazi
hilo, kwa sababu maelezo anaandika mwenyewe na wiki hii watakuwa
wameshawasilisha, hivyo aliomba apewe wiki mbili awe amewasilisha majibu
yao.
Jaji alihoji hayo maelezo ya awali
yatasilikishwa lini, wakati wiki ya kwanza ya Desemba, wadaiwa walikuwa
wameshapatiwa hati ya madai na jana alitegemea wanamalizia kuwasilisha.
Wakili Lukosi alidai wanakuja kuna
haja ya kuwasilisha mapema, lakini kuna mkono wa tatu wa kupata maelezo
ambayo ni ya mdaiwa wa kwanza, vielelezo vya mdaiwa wa pili tayari,
lakini Mwanasheria Mkuu wa Serikali vielelezo vyake ni vingi ambavyo
huwezi kusoma kwa mara moja.
Jaji alisema lazima wamalize kusikiliza maelezo ya awali, ili kesi iweze kupangiwa Jaji mwingine wa kuisikiliza.
Mtemvu amefungua kesi hiyo
akiiomba mahakama hiyo itengue ushindi wa Mtolea kwa madai ya kwamba
hakupata nafasi ya kurudia kuhesabu kura na hapakuwepo na majumuisho.
STORY NA FULL SHENGWE
0 comments:
Post a Comment