Waziri wa Nishati na Madini Profesa SOSPETER MUHONGO
amewahakikishia wananchi kote nchini kuwa atahakikisha wananchi ambao
hawajapata huduma ya umeme wanapata huduma hiyo haraka kupitia mradi
wakala wa umeme vijijini ili waweze kuanzisha miradi ya kiuchumi ikiwemo
viwanda vidogo.
Waziri MUHONGO amesema kwa sababu nchi inataka kukuza uchumi ikiwemo
suala la ujenzi wa viwanda hivyo ni lazima umeme nchini uwe wa uhakika
na wa bei nafuu katika maeneo yote nchini mijini na vijijini.
Ameeleza hayo katika Kikao cha Kazi Kati yake na wapiga kura wake
kutoka vijijini 68 lengo ni kujadili masuala ya uchumi na maendeleo
katika jimbo la MUSOMA Vijijini

0 comments:
Post a Comment