Saturday, December 19, 2015

kagamee
 


Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Rwanda anasema matokeo ya awali yanaonyesha kuwa wananchi wa taifa hilo wamepiga kura kuunga mkono marekebisho ya katiba ya nchi hiyo yanayolenga kuondoa kikomo cha uongozi wa nafasi ya Urais hatua itakayorefusha muda wa uongozi wa Rais wa sasa wa nchi hiyo Paul Kagame.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasema 98% ya wapiga kura wameunga mkono marekebisho hayo ya katiba ambayo yatamruhusu Bw Kagame kuwania kwa muhula mwingine mwaka 2017, baada yake kumaliza muhula wa pili.

Rais Kagame alishika uongozi wa nchi hiyo tangu mwaka 1994 baada ya kumalizika kwa mauaji ya halaiki nchini humo ambapo inadaiwa kuwa amekuwa akisifiwa kwa kufanikiwa kuleta hali ya utulivu na kuwezesha kukua kwa uchumi lakini pia amekuwa akilaumiwa kwa kukandamiza upinzani na ukiukaji wa haki za binadamu .

Wakati hayo yakijiri mataifa ya magharibi yamekuwa yakimtaka Bw. Kagame kuonyesha mfano wa kuigwa nchi za Afrika pindi wanapomaliza muhula wa uongozi ili kuondoa migogoro inayotokea baada ya uchaguzi kama ilivyo nchini Burundi hivi sasa.

0 comments:

Post a Comment