Jumla ya Wanafumzi 7I0 wa shule ya msingi Sunzula ( A) wilayani
Itilima mkoani Simiyu walazamika kutumia tundu moja la choo na Walimu
ambapo mahitaji ya choo ni matundu 28 hali ambayo imesababisha kukwama
kwa ufundishaji na ujifunzaji na pia inaweza kusababisha milipuko ya
magonjwa,hivyo jitihada zinahitajika kabla shule hiyo kufunguliwa
januari mwakani .
Wakiongea na waandishi wa Habari walimu wa shule hiyo wamesema kuwa
baada ya choo cha wanafunzi kuanguka, wanafunzi hao hawakuwa na njia
mbadala ya kupata huduma hiyo na badala yake walilazimika kwenda porini
kabla ya kupewa choo cha walimu.
Wamesema kuwa baada ya kugundua kushuka kwa mahudhurio ya wanafunzi
shuleni hapo na chanzo kikiwa ni ukosefu wa vyoo vya wanafunzi, walimu
walilazimika kukigeuza choo cha chao chenye tundu moja kutumika kwa
wanafunzi wa jinsia zote.
Kwa upande wake Mbunge wa Itilima Njalu Silanga ambaye yuko katika
ziara jimboni mwake kujionea changamoto zilizopo aliyepita shuleni hapo
amesema yeye atamalizia choo hicho kwa kujenga boma na kupaua lakini
ameitaka jamii ya eneo hilo kuhakikisha inamalizia kwa kuyafunika
matundu hayo vizuri ili yeye amalizie.
0 comments:
Post a Comment