Sunday, December 6, 2015

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna mstaafu Alfred Tibaigana amesema Rais John Magufuli amepatikana wakati sahihi, kwa kuwa nchi inamhitaji kiongozi ambaye akitoa amri inatekelezwa mara moja. Kauli ya Tibaigana inakuja takribani miezi 15 tangu aliposema anatamani kuiona Tanzania ikimpata rais dikteta kwa kuwa nchi haiwezi kupiga hatua iwapo mkuu wa nchi hataweza kukemea na kutoa amri watu wakatii.  

0 comments:

Post a Comment