Tuesday, December 8, 2015

 


MCHAKAMCHAKA wa kusafisha uozo katika ofisi za umma sasa umekuwa katika mtazamo tofauti,ambapo sasa mabosi katika ofisi hizo ndiyo wamekuwa wakiwadhibu wafanyakazi walioko chini yao ili kuepuka kuonekana wazembe.

Zikiwa zimepita siku chache toka Kamishna Mkuu wa TRA ,Rished Bade kusimamishwa kazi na Rais Magufuli,aliyeikaiumu nafasi yake katika ofisi ya kamishna Mkuu wa TRA Dr Philiph Mpango ameanza kuisafisha mamlaka hiyo .

Katika taarifa  yake kwa vyombo vya habari,Mpingo amemsimamisha kazi mkuu wa forodha wa TRA Patrick Mgoya kwa kile alichosema kuwa ni uzembe na kutowajibika ipasavyo katika nafasi hiyo


0 comments:

Post a Comment