Tuesday, December 8, 2015

 

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amefunguka kuwa anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kuwapigania watu walio chini yake katika kero mbalimbali zinazowakabili.

Makonda anayesifika kwa kuchapa kazi amesema kuwa ni jambo la fahari kwake kufanikisha kutatau mgogoro wa kimaslahi uliokuwa ukikikumba kiwanda cha Urafiki.

Katika taarifa yake kupitia ukurasa wake wa kijamii wa instagram,Makonda ameeleza jinsi alivyopambana hadi kufanikisha wafanyakazi wa kiwanda hiko kulipwa mshahara wa 150,000 kutoka 80,000 kwa mwezi

0 comments:

Post a Comment