Umoja wa Mataifa umesema wakuu wa
serikali ya Burundi na viongozi wa upinzani wanajaribu kuigawanya nchi
hiyo kwa misingi ya kimbari.
Mshauri maalum wa umoja huo kuhusu
mauaji ya kimbari Adama Dieng amesema matamshi yanayotolewa ni sawa na
yaliyokuwa yakitolewa kabla ya kutokea kwa mauaji ya kimbari katika
taifa jirani la Rwanda 1994.
Bw Dieng ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati.
Watu
240 wameuawa nchini humo tangu Rais Pierre Nkurunziza atangaze atawania
urais kwa muhula wa tatu mwezi Aprili. Alishinda uchaguzi.
Msemaji wa serikali Willy Nyamitwe, ametetea serikali akisema inakabiliana na magaidi.
“Mashambulio
ya kigaidi yanaweza kutokea Burundi na pahali popote duniani. Hii haina
maana kwamba Burundi haina amani,” Bw Nyamitwe amesema.
Tunapigana dhidi ya watu wanaojaribu kuleta ukosefu wa usalama nchini
mwetu. Tunawapokonya raia silaha ambazo wanashikilia kinyume cha
sheria, lakini baadhi wanafanya mambo kama magaidi. Kwa hivyo hili
halifanyiki Burundi pekee, hata Ulaya, na Marekani.”
Msemaji huyo amesema wapinzani wanaua wafuasi wao ili kuiharibia sifa serikali.
“Wanajua wapinzani wakiuawa, watu watadhani ni serikali inayowaua,” amesema Bw Nyamitwe.
0 comments:
Post a Comment