Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amesema
serikali inatarajia kukusanya kiasi cha Sh. trilioni 1.3 ndani ya mwezi
huu pekee.
Aidha, amesema ili kuhakikisha serikali inapata mapato ya
kutosha, atasimamia vyema suala la kukusanya kodi zinazostahili na
kutengeneza mazingira ya watu kulipa kodi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika viwanja vya
Ikulu mara baada ya kuapishwa, Dk. Mpango alisema kwa kipindi cha mwezi
mmoja serikali inaweza kukusanya kiasi hicho cha fedha.
“Nimekaa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kipindi
cha wiki tatu, nimeona kuwa kiasi hiki cha Sh. trilioni 1.3 kinaweza
kukusanywa. Kwa wiki iliyopita ya sikukuu, niliona makusanyo ni mazuri
na mpaka ifikapo mwisho wa mwezi huu, tutatimiza kiasi hicho,” alisema.
Namna ya kukuza Uchumi wa Nchi
Dk. Mpango, alisema ili kukuza uchumi wa nchi ni lazima
kuwa na utaratibu wa kujenga viwanda vikubwa nchini vinavyozalisha kwa
wingi jambo litakaloongeza pato la taifa.
“Nchini kwa sasa kuna kiwanda kimoja kikubwa cha Bia cha
Breweries (TBL) ambacho ndicho tunakitegemea ndio maana bei ya vileo
vinapanda kila siku. Lakini vingekuwapo kama hivyo 10, nina uhakikisha
tungekusanya mapato ya kutosha,” alisema.
Aibu ya kuomba misaada nje
Dk. Mpango, alisema miongoni mwa mambo yanayomnyima raha ni safari za kwenda ughaibuni kuomba misaada kwa nchi wahisani.
Alisema kitendo hicho ni cha aibu na kwa muda mrefu
kimekuwa kikimsonesha moyoni hasa kwa kuwa anafahamu kuwa taifa lake
lina utajiri mkubwa.
"Nimekwenda nje mara nyingi nikiongozana na mawaziri wa
fedha waliopita kwenda kuomba misaada.Huwa najisikia aibu
sana,tunadhalilika sana.
"Hatuna sababu ya kuwa ombaomba,tunachotakiwa kukifanya
ni kuimarisha mfumo wa ukusanyaji kodi na kuwaondolea mzigo wananchi wa
hali ya chini," Alisema Dr. Mpango

0 comments:
Post a Comment