Tuesday, January 19, 2016






Hivi karibuni kumezuka mjadala mpana kwenye mitandao ya kijamii hasa kwa wapenzi wa burudani nchini, baada ya vyombo mbalimbali vya habari kuripoti kuwa Diamond Platnumz anauwezo wa kuidhinisha upigwaji wa vichupa wa wasanii wa Bongo kwenye kituo cha MTV na akiamua zisipigwe anaweza kufanya hivyo.diamond akiwasha moto jana

Mjadala huo ulifika mbali mpaka kumuhusisha nguli huyo wa Afro Pop kuwa yeye ndiye kizuizi kikubwa cha nyimbo za msanii Alikiba kupigwa katika kituo hicho kikubwa cha MTV.nini


Kwa upande wake Alikiba baada ya kupata taarifa za kuwa Diamond ndiye anahusika katika kuidhinisha uchezwaji wa video za wasanii wa Bongo amefunguka na kueleza kuwa kama ni kweli MTV watakuwa wanakosea, kwa sababu wasanii wa ndani wanafanya vichupa vikali vinavyo wagharimu, hivyo akitokea mtu kuzibania inakuwa sio kitu kizuri.Babu-Tale (1)


Kwa upande wa Menejimenti ya Diamond Platnumz wamelizungumzia suala hilo na kueleza kuwa, halina ukweli wowote bali watu walimuelewa vibaya Diamond Platnumz kipindi anaelezea suala la mchango wake kwa wasanii wa ndani,  katika mahojiano yake na mtangazaji wa kipindi cha Papaso Dijaro Arungu cha TBC FM.djaro


Menejimenti ya Diamond Platnumz imeongeza na kueleza kuwa kama Diamond angekuwa anatoa idhini ya uchezwaji wa video za wasanii wa ndani, basi nyimbo za wasanii waliokaribu na Diamond zingepigwa huko kwa mfano Harmonize, Yamoto Band, Madee na wengineo.harmonize



0 comments:

Post a Comment