Tuesday, January 19, 2016

 
 
Naibu spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Tulia Ackson ameyata madhehebu ya dini nchini kuendelea kuliombea taifa na viongozi wake ili waweze kuwatumikia watanzania kwa usawa na uadilifu pamoja na kuliombea taifa mungu aliepushe na janga la kipindupindu linaloikabili baadhi ya mikoa ikiongozwa na mkoa wa Morogoro.

Dokta Tulia ametoa wito huo mjini Morogoro wakati wa kumtunuku tuzo ya Heshima askofu mkuu wa kanisa la TAG Dokta Barnabas Mtokambali kwa kutambua mchango wake wa maendeleo katika jamii tuzo iliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Weis Man la hapa nchini ambapo Dokta Tulia amesema jitihada zilizofanyika kuliombea taifa wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana ziendelee kwani viongozi wanawakati mgumu wa kuhakikisha Tanzania inakua kiuchumi.
 
Akipokea tuzo hiyo  askofu mkuu wa TAG askofu Dokta Barnabas Mtokambali ameshukuru shirika hilo kwa kutambua umuhimu wake katika kusaidia jamii ambapo kufuatia mkoa wa Morogoro kuongoza kwa kuenea kwa kasi ugonjwa wa kipindupindu askofu Mtokambali amewataka wananchi kuzingatia kanuni za usafi wa mazingira na chakula ili kutokomeza mlipuko huo.
 
Katika misa hiyo naibu spika Dokta Tulia Ackson ameshiriki maombi ya kuliombea bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalotarajia kuanza mapema Januari 26 mwaka huu.
 

0 comments:

Post a Comment