Wednesday, January 20, 2016

ISLAMIC STATE Wathibitisha Kifo cha "CHINJA CHIJA JOHN".
 
Kundi la Islamic State limethibitisha kwamba mwanamgambo aliyetafutwa sana na mataifa ya Magharibi, aliyejulikana kama Jihadi John, alifariki. Kundi hilo limetangaza kifo chake kwenye jarida lake la mtandaoni kwa jina Dabiq.

 

Mwanamgambo huyo aliuawa kwenye shambulio lililotekelezwa kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani Novemba mwaka jana.
Mwanamgambo huyo wa Islamic State aliyekuwa Maarufu kwa Ukatili wake Jina na lake halisi ni Mohammed Emwazi na ni raia wa Uingereza.
 

1988: Azaliwa Kuwait.
 

1994: Ahamia Uingereza
 

2009: Afuzu na shahada ya kwanza katika masuala ya kompyuta chuo kikuu cha Westminster
 

Agosti 2009: Asafiri Tanzania na marafiki zake wawili lakini wanazuiwa kuingia katika uwanja wa Dar es Salaam. Wanapandishwa ndege ya kuelekea Amsterdam, Uholanzi. Huko baada ya kuhojiwa, arejea Dover
 

Sept 2009: Aenda Kuwait kuishi na familia ya babake

Julai 2010: Arejea Uingereza kukaa kwa muda tu lakini ananyimwa visa ya kurejea Kuwait.
 

2012: Apita mtihani wa Celta wa kufundisha lugha ya Kiingereza
 

2013: Abadilisha jina lake na kuwa Mohammed al-Ayan. Ajaribu kusafiri Kuwait lakini anazuiwa. Atoweka. Wazazi wake waripoti kwa polisi kwamba hajulikani aliko. Polisi waambia familia miezi mine baadaye kwamba alienda Syria.
 

Video za mauaji alizoonekana
 

Agosti 2014: Video ya kuuawa kwa mwanahabari wa Marekani James Foley
 

2 Septemba 2014: Video inayoonyesha mwanahabari wa Marekani Steve Sotloff iakikatwa shingo
 

13 Septemba 2014: Video ambayo inaonyesha mfanyakazi wa misaada wa Uingereza David Haines akikatwa shingo
Oktoba 2014: Video ambako mfanyakazi wa misaada kutoka Uingereza Alan Henning anaonekana akikatwa shingo
 

Novemba 2014: Video ambayo Jihadi John anaonyeshwa akimuua mwanajeshi wa Syria. Kadhalika, inaonyesha mwili wa mfanyakazi wa misaada wa Marekani Abdul-Rahman Kassig, anayejulikana pia kama Peter Kassig
 

20 Januari 2015: Video ambayo Jihadi John anaonekana akisimama na mateka wawili wa Japan akidai kulipwa kikombozi ili waachiliwe huru
 

31 Januari 2015: Video inatolewa ikionekana kuonyesha Jihadi John akimkata shingo mateka Mjapani Kenji Goto.

1 comment: