Tuesday, January 19, 2016

4
 


Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano prof.MAKAME MBARAWA , amewataka makandarasi wanaojenga barabara  za MANGAKA MTAMBASWALA na MANGAKA NAKAPANYA  zilizopo  katika wilaya ya NANYUMBU mkoani MTWARA , kuongeza kasi ya ujenzi ili kuhakikisha barabara hizo zinakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa .
Prof.MBARAWA ametoa wito huo mkoani MTWARA mara baada ya kutembelea barabara hizo zenye jumla ya kilometa  miamoja thelathini na mbili, zinazojengwa kwa kiwango cha lami na kueleza kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo, ikilinganishwa na  muda uliobaki  kwa mujibu wa mikataba yao na serikali.
Akiwa katika Wilaya ya NANYUMBU , waziri MBARAWA  ametembelea mradi wa barabara ya MANGAKA MTAMBASWALA nyenye  jumla ya kilometa  sitini na tano nukta tano,  ambapo mhandisi mkazi wa mradi huo  ANORD MSENGEZI amemueleza waziri huyo kuwa  hadi sasa ujenzi umekamilika kwa  asilimia arobaini na tano.
Aidha  prof. MBARAWA pia ametembelea mradi wa barabara ya MANGAKA NAKAPANYA  yenye urefu wa kilometa sabini nukta tano na kuelezwa kwamba hadi sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia hamsini na tatu.
Kwa upande wake meneja wa wakala wa barabara TANRONDS mkoa wa MTWARA mhandisi  AISHA SALIM amesema wakala huo utafuatilia na kusimamia kwa karibu makandarasi hao, kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa wakati na kwa  ubora unaotakiwa.

0 comments:

Post a Comment