IKIWA imepita siku moja toka Serikali itangaze kuilima faini ya bilioni 3 benki ya Stanbic kutokana na kuhusika katika sakata la hati fungani yenye thamani ya trilioni 1.3,Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ameibuka na hoja ya kuitaka Serikali iichukulie hatua zaidi benki hiyo kwa kuhusika na sakata la kutakatisha pesa za akaunti ya Tegeta Escrow.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook,Zito aliandika haya
Benki Kuu imeitoza Benki ya Stanbic faini ya tshs 3bn kufuatia kuhusika kwake na sakata la #Hatifungani ya tshs 1.3trn.
Hata hivyo mwaka umekatika Benki Kuu haiajaueleza umma hatua gani ilichukua dhidi ya Benki hiyo ya Stanbic kuhusu kuhusika kwake na utakatishaji wa fedha za akaunti ya #TegetaEscrow. Watanzania wana haki ya kujua
Benki Kuu imeitoza Benki ya Stanbic faini ya tshs 3bn kufuatia kuhusika kwake na sakata la #Hatifungani ya tshs 1.3trn....
Posted by Zitto Kabwe on Sunday, January 17, 2016

0 comments:
Post a Comment