imebainika kilichopelekea Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kukwama kupanga tarehe ya uchaguz wa marudio katika kikao kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Taarifa za uchunguzi zilizopatikana jana mjini Zanzibar na kuthibitishwa
na baadhi ya makamishina wa tume hiyo, zimedai kuwa tarehe ya kufanyika
uchaguzi huo ilikwama kupangwa baada ya tume kugawanyika makundi
mawili, wanaokubali kurudiwa na wanaopinga kufanyika uchaguzi huo.
Inadaiwa katika kikao hicho cha siku mbili kilichofanyika makao makuu ya
ZEC Maisara, mjini Zanzibar, tume hiyo ilishindwa kufikia muafaka wa
pamoja wa kupanga tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio baada ya
kuibuka mvutano.
Akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, Kamishina mmoja wa tume hiyo
ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake, alidai ajenda ya uchaguzi mkuu
haikupelekwa rasmi katika kikao hicho, isipokuwa ilipenyezwa na waziri
mmoja wa zamani.
Alisema baada ya kamishna huyo kutoa hoja ya kurudiwa uchaguzi, baadhi
ya makamishina walipinga, wakitaka kufahamu sababu za kurejewa uchaguzi
huo kama zimezingatia matakwa ya Katiba na sheria au unarudiwa kwa
sababu za kisiasa.
Aidha, alisema wajumbe hao walifika mbali zaidi na kutaka tamko la
Mwenyekiti wa ZEC la kufuta matokeo ya uchaguzi liwasilishwe katika
kikao cha tume ili lijadiliwe ikiwamo kuangali kama lina nguvu za
kikatiba na sheria.
“Kutokana na hali hiyo, ZEC imelazimika kuitaka kamati tendaji yake
(Sekretarieti) kuandaa mpango kazi wa kurudiwa kwa uchaguzi na kuonyesha
utaratibu mzima utakaotumika katika uchaguzi huo,” alisema.
Aliongeza kuwa, taarifa ya kamati tendaji itawasilishwa kwa tume na
kujadiliwa na kikao hicho ndiyo kitakachopanga tarehe ya kufanyika
uchaguzi huo baada ya kupatikana muafaka.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment