Posted by Williammalecela.com on Wednesday, January 13, 2016
Icon wa Bongo flava Naseeb
‘Diamond’ Abdul, amewashangaa wasanii wanaomtupia maneno kila kukicha
kuwa anawabania wasanii wengine ‘connections’ za kung’ara kimataifa.
Diamond Platnumz amesema
anasikitishwa sana na maneno hayo ilhali anafanya juhudi kubwa
kujitafutia na kuwatafutia wasanii wengine masoko ya kimataifa.
“Mi nashangaa sana kusikia
hayo maneno, wanasema hivyo wakati mi najitahidi kuwasaidia wenzangu
tutoboe wote, kila kolabo ya msanii wa nyumbani na msanii wa Nigeria
inayofanywa mi ndo huwa nasababisha.” alisema Diamond
“Nikiamua kubana mbona
naweza tu, kwa sababu vituo vingi vya nje vinanisikiliza kwa mfano tu
MTV wenyewe wakipokea video ya msanii yoyote kutoka hapa (Tanzania)
wananipigia wananiuliza kwanza huyu vipi? tuicheze ngoma yake au? mi
huwa nasema tu anafanya vizuri huku, basi inapita wanaicheza nikiamua
kubana si naweza tu?”
Katika ‘line’ nyingine, baba
Tiffah amesema timu yake ya Wasafi ndiyo iliishauri kituo cha tv cha
Nigeria Sound City na MTV kuanzisha chati za Afrika Mashariki kwenye
vituo hivyo
0 comments:
Post a Comment