Posted by Williammalecela.com on Sunday, January 17, 2016
Msanii nyota wa Bongo Fleva Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz au SIMBA amefunguka juu ya ushiriki wa mama yake mzazi kwenye video yake mpya ya Utaipenda.
Akizungumzia suala hilo Diamond Platnumz (SIMBA) amesema hakutegemea kama mama yake mzazi angekubali kushiriki katika video hiyo maana amekuwa akikataa hata kuhojiwa na vyombo vya habari kutokana na kutokuwa huru akiwa mbele ya kamera.
Diamond ameeleza kufurahishwa kwake na mama yake kushiriki katika video yake ya Utaipenda maana kusingekuwa na maana kama asingeshiriki kwasababu amemtaja sana kwenye verse ya pili.
0 comments:
Post a Comment