KAMATI Maalumu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliyoundwa na
Wizara ya Nishati na Madini, imezikatia umeme kampuni 24 za wawekezaji
katika migodi ya madini ya Tanzanite, baada ya kugundua wamechezea mita
zao na kulisababishia shirika hilo hasara ya zaidi ya shilingi milioni
157.
Akizungumza jana kwenye migodi hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, John
Manyema alisema kuwa zoezi hilo wamelifanya ndani ya kipindi cha Desemba
3 hadi Januari mwaka huu.
Alisema tayari wameshatembea katika eneo la Bagamoyo, Tanga, Dar es
Salaam na Manyara na kote wamebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na
wateja wa Tanesco.
Manyema alisema wamebaini tatizo kubwa katika migodi hiyo ni wizi
mkubwa wa umeme na kuahidi kuendelea na ukaguzi mara kwa mara. “Wahusika
wote tumewapa adhabu ya kuwakatia umeme katika migodi yao na kisha
tumewataka kumfuata Meneja wa Tanesco Mirerani ili warekebishiwe mita
zao,”alisema na kuwaonya wananchi kutojaribu kuhujumu shirika hilo kwa
namna yoyote, kwani lazima watakamatwa na watapata adhabu stahiki.

0 comments:
Post a Comment