Halfa
ya kuapishwa kwa makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu 26 iliyofanyika
jana Ikulu Jijini Dar es Salaam ilikuwa ya aina yake kutokana na kuapa mara mbili, huku Rais John Magufuli akiwaeleza kuwa asiyeweza kazi aseme asile kiapo, akae kando.
“Inawezekana
tulizungumza kwa ujumla lakini kumbe si wote wanakubali masharti kuhusu
rushwa, kutoa vitu vya upendeleo. Kwa hiyo, niwaombe makatibu wakuu
pamoja na kwamba mlishaapa kwangu, ambaye hakubaliani na hilo asimame
kando ili waliobaki waendelee,” alisema Rais Magufuli kabla ya kiapo cha pili cha uadilifu.
Hakuna aliyesema hawezi kazi hivyo wote walikula kiapo hicho.
Baada ya hapo, Balozi Sefue aliwataka kunyanyua mikono yao juu na kusoma
kiapo hicho cha uadilifu kwa sauti: “Mnakula kiapo hiki kulingana na makubaliano,
kwamba ukiwa mtumishi wa Serikali lazima ukubali kusaini fomu hii
inayoashiria kuwa kiongozi ana dhamana kubwa kwa nchi na wananchi.”

0 comments:
Post a Comment