MBUNGE wa Kilwa Kusini kwa tiketi ya CUF, Selemani Bungara ‘Bwege’
amesema Rais John Magufuli anatakiwa kuwajibika iwapo kutatokea
machafuko visiwaniZanzibar kutokana na kurudiwa uchaguzi.
Bungala amesema kurudiwa kwa uchaguzi Zanzibar ni mipango ya CCM kujihakikishia ushindi.
Amesema ni ukweli usiopingika kwamba serikali inayoundwa na CCM
imeamua kukanyaga demokrasia na sheria za uchaguzi na badala yake ubabe
ndio unaofanyika.
“Uchaguzi huu ni batili kwani kufutwa kwa uchaguzi ilikuwa ni kinyume
na sheria na katiba hata hivyo kurudiwa kwa uchaguzi tena ni kuvunja
Demokrasia.
“Hawa jamaa wameshapanga ushindi na hili siyo jambo geni, CCM
wamekuwa wakipora ushindi kwa maana hiyo hakuna jambo la ajabu kwani ni
kawaida ya CCM kutumia mabavu.
“Hapa hakuna amani ila kuna ubabe na ikitokea kukawepo na machafuko
mtu ambaye atatakiwa kushitakiwa ni rais, kwani amekaa kimya bila kutoa
tamko lolote licha ya kwamba taasisi mbalimbali na vyama vya siasa
kupiga kelele juu ya kutafuta ufumbuzi juu ya uchaguzi huo,” amesema
Bungala.

0 comments:
Post a Comment