NJAA KALI! Wadada wanaojihusisha na biashara ya kuuza miili yao
maarufu kama machangudoa, wameibuka na kupaza sauti kuwa kasi ya Rais
John Magufuli ikiwa ni pamoja na kukomesha ufisadi kwa staili ya
kutumbua majipu, imewanyoosha kwani wateja sasa wameanza kuadimika.
Wakizungumza jijini Dar kwa nyakati tofauti, akina dada hao walisema
wateja wao wakubwa walikuwa ni watumishi wa serikali, lakini hivi sasa
wameadimika, kwa wengine kufukuzwa kazi au kubanwa kwa mianya
iliyowapatia fedha nyingi isivyo halali.
“Kimsingi ni kwamba Rais Magufuli ametunyoosha, wateja wamepungua
sana na hata wachache wanaopatikana, kiasi cha fedha wanachotupatia ni
tofauti kabisa, inawezekana kabisa wengi wao ni waathirika wa tumbua
majipu inayoendelea, kama hakutakuwa na mabadiliko, itabidi kuangalia
namna nyingine ya kuishi,” alisema Feb Nayi anayepatikana Sinza Afrika
Sana.
Katika viunga vya Mwananyamala, mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa
jina moja la Aisha, alisema oparesheni tumbua majipu inawaathiri watu
wengi, tofauti na baadhi ya watu wanavyofikiria.
“Watu wanatumia kwa uangalifu sana, kwanza hawana uhakika na kesho
yao. Zamani nilipata elfu ishirini kwa tendo moja la haraka, lakini sasa
hivi hali imekuwa ngumu hadi elfu tano hauiachi,” alisema Aisha
anayefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka mitano sasa.
Kilio cha kukosekana kwa wateja wa maana kilikuwa pia kwa machangudoa
wa maeneo mengine waliohojiwa kama Buguruni, Manzese, Kariakoo,
Kigamboni, katikati ya jiji na maeneo ya pembezoni yaliyo maarufu kwa
biashara hiyo.
0 comments:
Post a Comment