Geita. Aliyekuwa Mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita,
Victor Swai; Mlipa fedha, Sundi Makonda na Ofisa Mipango, James Masolo
wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Geita na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakikabiliwa na
makosa mawili ya uhujumu uchumi, likiwamo la wizi wa zaidi ya Sh31.6
milioni.
Mwanasheria wa Takukuru wa mkoa huo, Osborn Pais
akisaidiana na Augustino Mtaki, alidai mbele ya Hakimu Safina Simfukwe
alidai kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Oktoba 21, 2010.
Watuhumiwa
hao walikana mashtaka na kuachiwa baada ya kutimiza masharti kwa kila
mmoja kulipa nusu ya fedha wanazotuhumiwa kuiba au kuweka dhamana ya
mali yenye thamani hiyo na wadhamini wawili wenye mali au nusu ya fedha
hizo.
Hakimu Simfukwe aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 11, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali.
Hakimu Simfukwe aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 11, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali.

0 comments:
Post a Comment