RAIS Dk. John Magufuli ameendelea na uamuzi wake wa kutosafiri nje ya nchi huku akilazimika kutuma ujumbe wa kumwakilisha katika mikutano ya kimataifa.
Hatua hiyo inatokana na agizo lake alilolitoa Novemba 7, mwaka jana, ambapo alipiga marufuku safari za nje ya nchi kwa maofisa wa Serikali ila tu itakapokuwa lazima na kwa ruhusa ya Ikulu.
Kutokana na hali hiyo, safari hii amelazimika kumtuma Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili akamwakilishe katika mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), unaofanyika mjini Gaborone nchini Botswana.

0 comments:
Post a Comment